City, Liverpool zakamata usukani

39

Liverpool na Manchester City zimekamata usukani wa Ligi ya Premier baada ya Chelsea kuangusha pointi mbili katika sare yao ya 2-2 dhidi ya Manchester United uwanjani Stamford Bridge.

The Red Devils walionekana ni kama wanaponyoka na pointi zote tatu baada ya Anthony Martial kuwaweka kifua mbele kabla ya Ross Barkley kusawazisha katika dakika ya 96 na kuwaharibia karamu. Bao hilo lilisababisha vurumai kwenye eneo la benchi la kiufundi wakati mmoja wa wasaidizi wa kocha wa Chelsea Maurizio Sarri aliseherekea bao hilo mbele ya Jose Mourinho na wasaidizi wake. Hatua hiyo ilimlazimu Jose kujaribu kumfuata msaidizi huyo kabla ya kuzuiwa.

Jurgen Klopp na vijana wake wa Liverpool walipta ushindi wa 1-0 dhidi ya Huddersfield wakati Mohamed Salah alifunga bao la ushindi nao Manchester City wa Pep Guardiola wakawabumburusha Burnley kwa mabao 5-0. Kwingineko, Tottenham Hotspur waliwafunga West Ham 1-0 kupitia mkwaju wa Erik Lamela, Cardiff wakapata ushindi wao wa kwanza kwa kuwalaza Fulham 4-2, huku Bournemouth na Southampton zkitoka sare tasa. Newcastle bado wanatafuta ushindi baada ya kuangushwa 1-0 na Brighton, huku Wolves wakinyukwa 2-0 na Watford.

Author: Bruce Amani