City yashinda dhidi ya Real Madrid ugenini

Goli la Gabriel Jesus na Kevin de Bruyne la dakika za jioni kipindi cha pili zimeipa uongozi Manchester City katika mchezo wa ugenini wa mkondo wa kwanza wa Champions League dhidi ya Real Madrid katika mtanange uliopigwa dimba la Santiago Bernabeu hatua ya 16 bora.

Madrid walikuwa wa kwanza kufunga goli ngwe ya pili baada ya makosa ya walinzi wa City hatimaye Vinicius Junior akayatumia kumpasia Isco aliyekwamisha mpira wavuni, kisha wenyeji walipata nafasi nyingine nzuri ya kuongeza goli la pili pale ambapo Ramos aliingia katika 18 ya Manchester na kupiga shuti lililopotea mwelekeo.

Dakika 12 baadae mambo yalibadilika baada ya Jesus kufunga goli kwa kichwa akimalizia krosi ya Mendy.

City ambao walikuwa katika kiwango bora ugenini walipata goli la pili kwa penati baada ya ingizo jipya Raheem Sterling kuangushwa kwenye kisanduku cha 18 kisha De Brune akakwamisha mpira wavuni na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka dakika 90.

Mbaya zaidi kwenye mechi hiyo Madrid walimaliza mtay huo wakiwa pungufu kufuatia nahodha Ramos kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Jesus.

Unakuwa mchezo wa kwanza kwa Manchester City kushinda dhidi ya Real Madrid katika mashindano ya Klabu bingwa Ulaya, huku matokeo yakiwapa ahueni katika mchezo wa marejeano wakiwa vinara.

Mchezo wa marudiano utapigwa mwezi ujao.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends