City yashinda, Juve yatoa sare na Atletico pamoja na matokeo mengine

49
Mashindano ya Ligi ya Mabingwa michezo ya awali hatua ya makundi imemalizika ambapo kuna matokeo ya kushangaza na vipigo vizito vimehusika karata ya mwanzo.
Kufungwa kwa Real Madrid kumetikisa miamba ya Blancos, kipigo cha goli 6-2 cha zungumzwa pia.
Matokeo ya Jumatano.
Juventus imetoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Atletico Madrid katika mtanange uliopigwa dimba la Wanda Metropolitano, Hispania.
Magoli ya Juventus yamefungwa na Juan Cuandrado na Blaise Matuidi huku upande wa Atletico akifunga Stefano Savic na Hector Herrera.
Wanafainali wa msimu uliopita Tottenham Hotspurs imetoka nyuma goli 2-0 na kusawazisha kuwa 2-2 katika mchezo ambapo Spurs walikuwa na makosa mengi dhidi ya Olyimpiacos.
Baada ya vichwa kuwa chini mshambuliaji Harry Kane na Lucas Moura walifanya mashabiki wa Spurs kulipuka kote duniani.
Kwingineko, Bayern Munichen wakiwa dimba la Allianz Arena wameibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Crvena.
Manchester City wamepata ushindi mnono wa goli 3-0 dhidi ya Shaktar Donetsk.
Bayer Leverkusen wakiwa uwanja wa nyumbani wamekubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Locomotive Moscow ya Urusi.
Karata ya marejeano itafanyika wiki mbili kutoka sasa.

Author: Bruce Amani