Club Africain yapewa ushindi wa 3 – 0, Ismaily yatozwa faini

Klabu ya Club Africain imepewa ushindi wa mezani wa goli 3-0 na wapinzani wao wa Misri Ismaily wakatozwa faini ya Euro 35,000 baada ya mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika CAF mwezi uliopita kusimamishwa. Katika hatua nyingine CAF imetoa adhabu kwa Ismaily katika mchezo wake wa Jumamosi ya Feb 23 dhidi ya CS Constantine kutoka Algeria kuchezwa bila mashabiki.

Africain walikuwa wanaongoza 2-1 dhidi ya Ismaily katika mtanange uliopigwa Januari 18 kabla ya mashabiki kuanzisha vurugu ya kurusha makopo na mawe na hivyo refarii akaumaliza mchezo huo katika dakika za mejeruhi.

Ismaily iliondolewa kwenye mashindano hayo ya CAF kabla ya kupeleka rufaa iliyokakubaliwa na Shirikisho hilo la soka la Afrika. CAF ilifikia uamuzi wa kuiruhusu Ismaily ambayo imewai kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa kwa masharti kuwa hakutakuwa tena na matukio ya mashabiki kuvamia uwanjani

TP Mazembe kutoka Congo inaongoza kundi C kwa alama 7 ikifuatiwa na Constantine yenye alama 6 na Club Africain alama 4, wakati Ismaily ikiburuza mkia bila hata pointi moja.

Ismaily na Constantine zimecheza michezo michache zaidi ya timu nyingine kwenye kundi hilo ambapo zitalazimika kucheza michezo yao kwa mda mfupi ili kulingana mechi za kucheza. Mechi hizo zitachezwa Februari 23 na Marchi 2.

Katika hali ambayo imekuwa ikitoa hofu kwa watu wengi, Uwanja uliozuka hiyo sintofahamu utatumika kwenye mashindano ya AFCON mwaka 2019 kuanzia Juni na Julai.

Nchi ya Misri ilipata fursa ya kuandaa tamasha la AFCON baada ya Cameroon mwezi Januari kupokonywa kibali cha uenyeji baada ya kuchelewesha maandalizi. Kwa mara ya kwanza, kutakuwa na ongezeko la timu zitakazoshiriki kutoka 16 mpaka 24.

Mechi zilizo salia ni pamoja na:

Feb 23: Ismaily v Constantine

Mar 2: Constantine v Ismaily

Mar 8: Constantine v Africain, Ismaily v Mazembe

Mar 16: Africain v Ismaily, Mazembe v Constantine

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends