Constant Omari Selemani afungiwa kuwania Urais wa CAF kutokana na makosa ya kimaadili

Kaimu Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika – CAF, Constant Omari Selemani, amepoteza sifa ya kuwania nafasi ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho hilo na sifa ya kugombea nafasi ya kuwa mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Fifa baada ya kukutwa na tuhuma katika utendaji wake.

Kamati ya Fifa katika kupitia makosa ya watendaji katika taasisi zake siku ya Jumatano ilisema kuwa Omari Selemani amepoteza sifa ya kuwania nafasi hiyo kwa sababu kuna uchunguzi unaendelea dhidi yake hasa katika makosa ya kimaadili.

Awali Selemani aliweka wazi kuwa katika uchaguzi wa Machi 12, 2021 atawania nafasi ya ujumbe kwenye kamati ya Fifa ambapo kukutwa na shutuma hizo zinamuweka katika mazingira magumu ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kwa kawaida, unapokuwa mjumbe wa Halmshauri ya Fifa unakuwa tayari ni mjumbe wa kamati tendaji ya Caf, Selemani alitajwa kuwa Makamu wa Rais katika utawala wa CAF chini ya Rais wa wakati huo Ahmad Ahmad.

Uamuzi uliotolewa siku ya Jumatano unakuja ikiwa ni miezi michache tangia Ahmad afungiwe kujihusisha na shughuli za soka.

Ahmad alifungiwa miaka mitano na Fifa Novemba mwaka Jana baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares