Conte amtaka Ndombele atumia kipaji chake Tottenham

Kocha mpya wa Tottenham Antonio Conte amemwambia kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Tanguy Ndombele kutumia kipaji chake kwa manufaa ya klabu na siyo kucheza kwa ubinafsi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka, 24, ambaye alisajiliwa kwa kiwango kikubwa cha fedha katika usajili bado hajafikia thamani ya kile ambacho dau la pauni milioni 53.8 lilitumika.

Ndombele anaweza kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Leeds United wakati ambao Oliver Skipp amesimamishwa.

“Nilikuona naona Waalimu wengi wanapata shida namna ya kumchezesha hasa eneo ambalo litamfaa zaidi”, alisema kocha Conte ambaye amewai kufanya kazi Inter Milan na Chelsea.

“Tanguy ni mchezaji bora mwenye kipaji kikubwa. Lakini anatakiwa kujua lazima acheza kama timu inavyohitaji, msingi ni kufanya lile nafasi inalolihitaji”.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends