Conte apata ushindi wa kwanza Spurs mbele ya Leeds United

Kocha Antonio Conte amekiongoza kikosi cha Tottenham Hotspur kushinda mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England baada ya kuifunga goli 2-1 Leeds United mchezo uliopigwa Leo Jumapili Novemba 21.

Spurs imelazimika kutokea nyuma kwa bao 1-0 na kushinda kupitia bao za kipindi cha pili ukiwa ni ushindi muhimu kwa kocha mrithi wa Nuno Espirito Santo, Conte.

Bao la Leeds United ya Marcel Bielsa limefungwa na winga wa kimataifa wa Wales Daniel James akimalizia krosi maridhawa ya Jack Harrison.

Hata hivyo, goli la kiungo mkabaji Pierre-Emile Hojbjerg baada ya kazi kubwa ya Lucas Moura na lile la beki wa kushoto Sergio Reguilon yalitosha kuwapa alama tatu Spurs.

Ushindi huo unaifanya Spurs kukwea mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo alama nne kuingia nne bora Wakati Leeds United wakibakia nafasi ya 17.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends