Costa afungiwa mechi nne za Serie A

53

Winga wa Juventus Douglas Costa amefungiwa kucheza mechi nne za ligi kuu ya kandanda Italia – Serie A baada ya kumtemea mate Federico Di Francesco wakati wa mchuano wa Jumapili 16.09.2018

Juventus ilishinda mechi hiyo 2-1 licha ya Costa kutimuliwa uwanjani, kabla ya kuomba radhi kupitia taarifa baada ya mechi hiyo kutokana na tabia yake.

Ligi ya Italia imesema Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28, atakosa michuano dhidi ya Frosinone, Bologna, Napoli na Udinese lakini ataweza kucheza dhidi katika Champions League

Author: Bruce Amani