Dakika za nyongeza zaichinja Spurs 3-0 na kuwatupa nje ya Ligi ya Europa
Tottenham Hotspur wametolewa rasmi katika mashindano ya Ligi ya Europa baada ya kukubali kipigo cha goli 3-0 dhidi ya Dinamo Zagreb kwenye mechi ya raundi ya pili iliyopigwa Leo Alhamis Machi 18.
Wakitoka kuongoza bao 2-0 Spurs unaweza sema walikuwa na kazi rahisi kufuzu lakini haikuwa hivyo baada ya Mislav Orsic kufunga goli tatu pekee yake na kukowezesha kikosi cha Zagreb kusonga mbele hatua ya nane bora.
Kocha Jose Mourinho akiwa amefanya mabadiliko ya wachezaji saba amelipa gharama ya kutokuwa kwenye ubora kwa kikosi chake kufuatia bao hizo.
Dakika 90 zilikamilika kwa Zagreb kufunga bao 2-0 kwa maana hiyo kukawa na dakika za nyongeza ambapo Orsic akiwa katika ubora alifunga bao la 3 na kufanya matokeo kuwa 3-0, na matokeo ya jumla kuwa 3-2.
Baada ya Spurs kutupwa nje ya mashindano kesho Ijumaa Machi 19, 2021 watakuwa mashuhuda tu wa droo ya Ligi ya Europa hatua ya robo fainali.