De Bruyne abeba tuzo ya PFA kwa mara ya pili mfululizo na kufikia rekodi ya CR7

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne amefanikiwa kutwaa tuzo ya Chama cha Wachezaji kandanda la Kulipwa katika Premier League kwa msimu wa pili mfululizo.
Wakati de Bruyne akishinda tuzo hiyo, mchezaji mweza Phil Foden raia wa England ameshinda tuzo ya mchezaji kinda katika tuzo ambayo imetoka kwa beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold.
Wachezaji wote wawili walikuwa kwenye ubora mkubwa na kuisaidia Manchester City kushinda mataji mawili na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ingawa ilichapwa na Chelsea bao 1-0.
De Bruyne, 29, anakuwa mchezaji wa pili kutwaa tuzo hiyo mara mbili akifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Cristiano Ronaldo.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares