De Bruyne aingia kandarasi mpya Manchester City

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne ameingia mkataba mpya na waajiri wake hao mpaka mwishoni mwa mwaka 2025.

Kiungo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 raia wa Ubeligiji alikuwa na miaka miwili kwenye kandarasi yake ya awali.

De Bruyne ameshinda taji la EPL mara mbili, kombe la FA na Kombe la Ligi mara nne tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Wolfsburg ya Ujerumani mwaka 2015.

“Kuongeza mkataba mpya lilikuwa jambo rahisi kwangu, hii klabu inanipa kila kitu, kiwango kimeimarika maradufu hapa”, alisema de Bruyne ambaye amekuwa mhimili wa kocha Pep Guardiola kwa misimu zaidi ya minne sasa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares