De Bruyne akutwa na Covid-19

Kiungo mchezeshaji wa Manchester City Kevin de Bruyne amekutwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 baada ya mechi za kimataifa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, atatakiwa kujitenga mwenyewe kwa angalau siku 10 ambapo sasa atakosa mechi ya Jumapili dhidi ya Everton na mtanange wa Uefa dhidi ya Paris St-Germain Jumatano.

De Bruyne, ambaye tayari alishapata chajo ya Corona, alifunga goli la ushindi kwenye mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 akiwa na Ubeligiji.

Kocha wa kikosi hicho, Pep Guardiola amethibitisha kuwa atamkosa mchezaji huyo huku akisema huenda dalili hizo ni madogo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends