Dembele aipa Lyon pointi tatu katika derby dhidi ya Saint Etienne

Moussa Dembele ameiwezesha klabu ya Lyon kupata ushindi wa goli 2-1 katika dakika za lala salama dhidi ya Saint Etienne baada ya kukwamisha mpira kimiani. Romain Hamoura aliipatia goli la uongozi la Saint Ettiene kunako dakika ya 21 ya mchezo uliopigwa Stade Geoffroy Guichard, lakini Nabil Fekir aliisawazisha Lyon goli katika kipindi cha pili kwa njia ya penati baada ya Loic Perrin kunawa mpira.

 

Moussa Dembele ambaye alitokea bechi alifunga goli kwa kichwa baada ya kusahaulika kwa kutokabwa katika dakika za lala salama na kufanya Lyon kutakata kwa ushindi.

 

“Tulikuwa na shauku ya kushinda mchezo huu, kutokana na hisia zetu juu ya mchezo wa namna kama hii (Derby) wote tulicheza vizuri lakini timu iliyopata ushindi ndiyo ilicheza vizuri zaidi” Alisema kocha wa Lyon Bruno Genesio.

 

Matokeo hayo yameifanya Lyon kupanda mpaka nafasi ya tatu baada ya kufanikiwa kuwapa Saint Etienne kichapo cha kwanza nyumbani kwao.

 

Kwingineko Marseille ilipata ushindi wa kwanza wa goli 1-0 dhidi ya Caen katika Ligue 1 tangu Novemba licha ya kumpoteza Dimitri Payet kwa majeruhi.

 

Morgan Samson ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Payet aliupiga mpira kichwa kilichomkuta Kevin Strootman ambaye aliisaidia Marseille kupata alama 3 za kwanza.

 

Caen walicheza watu kumi karibia kipindi chote cha pili baada ya Frederic Gilbert kuonyeshwa kadi mbili za njano.

 

Marseille wamepanda mpaka nafasi ya saba, alama sita kuingia nafasi ya timu zitakazo shiriki ligi ya mabingwa.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments