Depay aipa alama tatu Barcelona kwa Getafe

43

Kikosi cha FC Barcelona kimepata ushindi wa goli 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga dhidi ya Getafe huku Memphis Depay akifunga goli la ushindi.

Sergi Roberto alianza kuwapa uongozi Barcelona kupitia pasi ya Jordi Alba kunako sekunde ya 99 pekee hata hivyo Sandro alisawazisha goli baada ya maelewano mazuri na Carles Alena.

Depay alifunga goli akitumia uwezo mzuri kwa ushirikiano na kiungo wa zamani wa Ajax Frenkie de Jong alipachika bao mbele ya mashabiki 26,000.

Ushindi huo unaifanya Barcelona kufikisha alama saba katika mechi tatu za awali wakati Getafe wakipoteza mechi zote tatu za La Liga.

Author: Bruce Amani