Depay awatoa udende Barcelona, ang’aa na Uholanzi

Winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay ameendelea kuwa na kiwango bora katika majukumu ya timu ya taifa ya Uholanzi kwa kufunga goli moja na kusaidia lingine katika ushindi wa bao 3-0 walioupata dhidi ya Georgia mchezo wa kirafiki kujiandaa na Euro 2020.
Depay, alifunga goli mbili kwenye mchezo uliopita dhidi ya Scotland siku ya Jumatano, goli lake lilikuwa la mkwaju wa penati kufuatia madhambi ndani ya eneo la hatari.
Mshambuliaji Wout Weghorst aliongeza bao la pili akimalizia mpira wa Depay likiwa ni bao lake la kwanza katika kandanda la kimataifa.
Kijana wa Ajax Ryan Gravenberch alifunga goli la tatu akimalizia mpira uliopanguliwa na mlinda mlango wa Georgia.
Sasa kocha wa Uholanzi ana kazi moja tu kujiandaa na mchezo dhidi ya Ukraine utakaopigwa Juni 13 kufuatia kuwa na matokeo rahisi.
Kundi D, mbali na Uholanzi kuna Austria, Macedonia Kaskazini pamoja na Ukraine.
Winga Depay ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya soka la Hispania Barcelona amekuwa na kiwango bora kama ishara ya kuthibitisha utofauti kwenye kusakata kabumbu la Ufaransa na Uholanzi.
Hata hivyo kwa sasa kocha Ronald Koeman amewekeza nguvu zake kumsajili kiungo mkabaji wa Liverpool Georginio Wijnaldum baada ya Sergio Kun Aguero.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares