Dewji atamba kufanya usajili mkubwa Simba

Siku nne tangia klabu ya Simba kufanya maamuzi ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Zacharia Hans Poppe aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Mwenyekiti mpya Kassim Dewji amesema ataongeza wataalam wawili wa usajili kwenye jopo lake tayari kwa usajili wa dirisha dogo la Desemba 15.

Kassim Dewji alithibitishwa kuwa Mwenyekiti wa Simba kwenye usajili kwenye mkutano Mkuu wa Simba uliofanyika Ukumbi Jumapili iliyopita kurithi mikoba ya Hans Poppe aliyefariki dunia.

Tuna maboresho ambayo tunataka kuyafanya katika Kamati ya usajili, tunaamini baada ya maboresho hayo kutakuwa na mabadiliko kwenye usajili wetu, na yatakwenda ndani ya Bodi kama yatapata ridhaa ya Bodi

Katika utaratibu wetu wa usajili tuna kanuni na taratibu zetu, mchezaji wa nje awe anacheza timu ya Taifa na pia tuangalie ukanda ambao anatokea mfano sehemu ambayo soka liko juu tunaangalia anacheza timu gani,” alisema.

“Wajumbe wengi waliopo kwenye kamati ya usajili nimeshafanya nao kazi ambao ni Mulamu Ng’hambi, Magori na Nassoro tunafahamiana na tumefanya kazi pamoja,” alisema.

Amesisitiza pia kuwa endapo kocha atahitaji mchezaji au wachezaji dirisha dogo watafanya hivyo huku akisisitiza kuwa ukanda wa Afrika mchezaji yeyote watakayemuhitaji atasajiliwa bila kizuizi chochote.

Dewji nafasi aliyopewa alisema sio mpya kwake aliyawahi kuwa Mwenyekiti kabla hajabadilishwa na kuwa mjumbe chini ya marehemu Zacharia Hans Poppe.

“Tulikuwa tunafanya kazi kwa pamoja vizuri kilichobadilika sasa ni kupanda nafasi tu nina uzoefu mkubwa kwenye sekta hiyo na mwaka huu nataka kufanya mabadiliko.”

Simba imekuwa ikihaha mpaka sasa kuziba nafasi ya Clatous Chota Chama na Luis Jose Miquissone ambao licha ya usajili uliofanyika dirisha kubwa la usajili la mwezi Agosti bado unaonekana kutofua dafu, miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa ni kurejeshwa kwa Chama “Mwamba wa Lusaka”.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends