Drogba ajitosa kinyang’anyiro cha rais wa chama cha soka Ivory Coast

400

Nguli wa kandanda aliyewapa burudani mashabiki wa Chelsea dimbani Stamford Bridge Didier Drogba amejitosa rasi katika kinyang’anyiro cha Urais wa chama cha soka cha Ivory Coast.

Drogba mwenye umri wa miaka 42, ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Afrika ni miongoni mwa wagombea wanne wanaotafuta ridhaa ya kukiongoza chama cha soka katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Hata hivyo, hana uhakika iwapo atashiriki katika uchaguzi huo uliopangwa Septemba 5.

Pamoja na kuhitaji uteuzi kutoka kwa vitatu kati ya vilabu 14 vya ligi kuu ya Ivory Coast na viwili kutoka ligi za daraja la chini, Drogba lazima apate idhini ya kundi lolote kati ya matano maalum: Makocha, madaktari, wachezaji wa sasa na wa zamani na marefarii.

Wote hawajatangaza wazi ni nani wanayemuunga mkono, na wagombea kwanza lazima wapigwe msasa na tume ya uchaguzi kabla ya kufuzu kugombea katika uchaguzi huo. Matokeo hayo yanatarijiwa katika siku tano zijazo kwa mujibu wa msemaji wa shirikisho la kandanda

Author: Bruce Amani