Dortmund watupilia mbali dili la Chelsea kwa Haaland

Borussia Dortmund imegairi kufanya biashara ya kumuuza mshambuliaji hatari raia wa Norwei Erling Braut Haaland kufuatia fedha nono kushindwa kutengwa na Chelsea ambayo ilikuwa inahusishwa kumsajili.

Licha ya dili hilo kuonekana kama kufa, inaelezwa kuwa Chelsea haikutuma ofa yoyote ya strika huyo anayetimiza miaka 21, tarehe Julai 21.
Bosi wa Chelsea Thomas Tuchel anahitaji huduma ya Haaland, ambaye alifunga goli 20 katika mechi 16 za Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Red Bull Salzburg na Borrusia Dortmund.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola pia amekuwa akihusishwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambaye amekuwa nuru Ulaya tangia akiwa Salzburg na sasa Dortmund.
Lakini Dortmund wamekuwa wagumu kukubali ofa yoyote kwa sasa inayomhusu Haaland, pengine ni kwa sababu imemtoa winga wa England Jadon Sancho kwenda Manchester United kwa ada ya pauni milioni 73.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares