Dortmund yabanduliwa nje ya Kombe la DFB

Vinara wa ligi kuu ya Ujerumani, Borussia Dortmund wameondolewa kwenye michuano ya kombe la Ujerumani, baada ya kutandikwa 4-2 kupitia mikwaju ya penalti na Werder Bremen katika hatua ya 16 bora jana Jumanne. Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikitoka sare ya mabao 3-3.

Max Kruse aliifungia Bremen penalti ya ushindi huku mlinda mlango wake Jiri Pavlenka akiokoa mikwaju ya penati ya Dortmund iliyopigwa na na Paco Alcacer na Maximillian Philipp.

Shuti la dakika ya 113 la Achraf Hakimi lilionekana kuwapa tikiti Dortmund katika mzunguko wa robo fainali lakini Martini Harnik wa Bremen alivuruga hali ya mambo baada ya kufunga bao dakika 6 baadae, na kupelekea mechi kuamuliwa na matuta.

Bremen inayoshikilia nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi ya Bundesliga, ilijipatia bao la kwanza katika dakika ya 5, kupitia Milot Rushica, lakini Kapteni Marco Reus wa Dortmund alisawazisha baada ya kupata free kick.

Christian Pulisic aliwapatia bao wenyeji bao la kuongoza 2-1 mwishoni mwa nusu ya kwanza ya muda wa nyongeza, lakini Claudio Pizzaro aliisawazisha Bremen na kuwaacha Hakimi na Harnik wakipigana makonde kabla ya mikwaju ya penalti.

Leverkusem walibanduliwe nje kwa kuzabwa 2 -1 na klabu ya daraja la pii Heidenheim. Timu nyingine ya daraja la pili Hamburg iliiondoa Nuremberg inayoshiriki daraja la kwanza. Bayern Munich watakutana na Hertha Berlin leo Jumatano.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends