Dortmund yachapwa na Freiburg Bundesliga

Freiburg imeitwanga Borussia Dortmund bao 2-1 katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga mtanange uliopigwa Leo Jumamosi Agosti 21.

Mabao bora kutoka kwenye kila ungwe yaliwapa uhakika Freiburg nafasi ya kuibuka kidedea mbele la Dortmund homa ya msimu

Magoli yakifungwa na Vincenzo Grifo na Roland Sallai kabla ya juhudi za Jude Bellingham katika kufunga goli kuishia kwa Yannik Keitel na hivyo kuonekana ni goli la kujifunga lakini la kufutia machozi kwa Dortmund.

Licha ya utawala mzuri wa mchezo, hawakuweza kupata matokeo chanya ambayo sasa yanawaacha na alama tatu kwenye mechi mbili za awali.

Wiki mbaya kwa Dortmund ambao katikati ya wiki walipoteza kwa Bayern Munich katika mchezo wa kuwania ubingwa wa Kombe la Ujerumani.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends