Dortmund yakabwa na Hoffenheim

Borussia Dortmund ilimudu kupata pointi moja dhidi ya Hoffenheim licha ya kumaliza mchezo na wachezaji kumi uwanjani. BVB ilikuwa nyuma bao moja kwa sifuri lililofungwa na Joelinton kabla ya kumuingiza uwanjani chipukizi wa Uingereza Jadon Sancho kujaribu kuokoa jahazi.

Mambo yaligeukwa kuwa mabaya kwa BVB wakati beki Mfaransa Abdou Diallo alipewa kadi nyekundu katika dakika ya 76.

Hata hivyo Dortmund walihakikisha kuwa wanaendeleza rekodi yao ya kutofungwa msimu huu baada ya Mmarekani Christian Pulisic kusukuma wavuni bao la kusawazisha ambalo ni lake la pili msimu huu.

Katika viwanja vingine Hertha Berlin walipanda kileleni angalau kwa muda baada ya kupata ushindi wa nyumbani wa 4-2 dhidi ya Borussia Moenchegladbach. Vedad Ibisevic aliifungia mabao mawili Hertha, ambao walikuwa wamefungwa bao kupitia penalty ya Thorgan Harzad.

Augsburg ilitoka nyuma mabao 2-0 na kuiduwaza Werder Bremen kwa mabao 3-2 huku nayo Nuremberg ikiizaba Hannover 2-0 na Freiburg ikaandikisha ushindi wake wa kwanza wa msimu kwa kuifunga Wolfsburg 3-1

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends