Dortmund yavuta alama tatu mbele ya Club Brugge ushindi wa 3-0

113

Erling Braut Haaland alitupia bao mbili katika ushindi wa goli 3-0 wa Borrusia Dortmund mbele ya Club Brugge ya Ubeligiji mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Haaland alitupia goli la kwanza kwa kumalizia pasi ya Jadon Sancho akifikisha magoli 12 zaidi ya zile rekodi zilizowekwa na Ruud van Nistelrooy na Roberto Soldado.

Winga qa kiingereza Sancho akafanya matokeo kuwa 2-0 kwa kutupia faulo bora nje kidogo ya 18. Haaland, 20, aliongeza bao la pili kwa upande wake la tatu kwa Dortmund goli hilo lilihitimisha matokeo ya 3-0.

Author: Bruce Amani