Dortmund yawika mbele ya mtani wake Schalke na kurejea katika mkondo wa ushindi

Klabu ya Borussia Dortmund imefanikiwa kurudi kwenye ubora wake kufuatia kuandikisha ushindi muhimu katika mchezo wa dabi wa goli 4-0 dhidi ya Schalke 04 mtanange wa Ligi Kuu nchini Ujerumani uliopigwa Jana Jumamosi.

Dortmund ambao walikuwa hawajapata matokeo chanya kwenye mechi tano kati ya sita zilizopita za Bundesliga walifanikiwa kurudi kwa kishindo na kupata goli hizo nne kupitia kwa Jadon Sancho, Erling Braut Haaland (goli 2) na Raphael Guerreiro.

Schalke, ambao wanabakia mwishoni mwa msimamo wa Bundesliga alama tisa kuelekea sehemu salama kwao, nafasi bora ilikuwa ungwe ya pili mwanzoni kabisa mpira wa kiungo Suat Serdar kugonga mtambaa wa panya.

Goli mbili za Haaland zinamfanya kufikisha bao 43 kwenye mechi 43 tangia ajiunge na Dortmund kutokea Red Bull Salzburg.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares