Droo ya Europa Ligi yafanyika, Arsenal, Rapid Vienna na Molde kundi moja

228

Droo ya Ligi ya Europa imetoka rasmi baada ya timu zote kujikatia tiketi ya kushiriki kufikia jana Alhamis, ambapo Mabingwa wa Kombe la FA klabu ya Arsenal imepangwa kundi B. Timu nyingine zilizopangwa na The Gunners ni pamoja na Dundalk, Rapid Vienna na Molde katika mashindano ya msimu wa 2020/21.

Tottenham wameingia kwenye kundi moja na mabingwa wa Bulgaria, Ludogorets, LASK na Royal Antwerp kundi J.

Leicester City watacheza dhidi ya Braga, AEK Athens na Zorya Luhansk.

Kundi H lina timu ya AC Milan, Lille, Sparta Prague na Celtic.

Rangers wapo kundi  D na Benfica, Standard Liege na Lech Poznan.

Makundi matatu yatacheza siku moja ya Octoba 22 siku ya Alhamis.

Arsenal wamefuzu makundi ya Europa Ligi baada ya kuifunga Chelsea mchezo wa fainali mwezi Agosti.

Droo nzima iko hivi;

Kundi A: Roma, Young Boys, Cluj, CSKA Sofia

Kundi B: Arsenal, Rapid Vienna, Molde, Dundalk

Kundi C: Bayer Leverkusen, Slavia Prague, Hapoel Beer-Sheva, Nice

Kundi D: Benfica, Standard Liege, Rangers, Lech Poznan

Kundi E: PSV Eindhoven, PAOK, Granada, Omonoia

Kundi F: Napoli, Real Sociedad, AZ Alkmaar, Rijeka

Kundi G: Braga, Leicester, AEK Athens, Zorya Luhansk

Kundi H: Celtic, Sparta Prague, AC Milan, Lille

Kundi I: Villarreal, Qarabag, Maccabi Tel-Aviv, Sivasspor

Kundi J: Tottenham, Ludogorets, LASK, Royal Antwerp

Kundi K: CSKA Moscow, Dinamo Zagreb, Feyenoord, Wolfsberger

Kundi L: Gent, Red Star, Hoffenheim, Slovan Liberec

Author: Bruce Amani