Droo ya hatua ya 16 bora Kombe la ASFC hii hapa

Hatimaye michezo ya raundi ya tano ya Kombe la Shirikisho la TFF ASFC imefikia tamati kwa kupata timu 16 ambazo zitaingia kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu robo fainali, nusu fainali mpaka fainali yenyewe.

Tamati hiyo ilikamilishwa na Azam dhidi ya Friend Rangers mchezo uliopigwa Jumatatu huku Azam wakifuzu kufuatia ushindi wa goli 3-1.

Baada ya mchezo huo ratiba kamili ya michezo ya kumi na sita bora hii hapa.

Mbeya city itakuwa nyumbani kumenyana na vijana wa Namungo Fc kutoka Lindi, mtanange utakaofanyika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

 Timu ya daraja la kwan za Ihefu Fc itakutana na upinzani mkuu kutoka kwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo Azam Fc ambao katika miaka ya karibuni wameibuka kama timu pinzani kwa Simba na Yanga.

Klabu ya Jeshi la Kujenga nchi (JKT Tz) itakuwa katika dimba lao la Isamuhyo kucheza dhidi ya wanafunzi wa Alliance kutoka Mwanza.

Yanga watakuwa katika dimba la Taifa kucheza dhidi ya timu ya daraja la kwanza Gwambina.

Timu yenye ustadi mkubwa katika kuutumia mpira Kagera Sugar watakuwa dimba la Kaitaba dhidi ya Kinondoni Municipal Council.

Hapa timu zenye uwezo sawa kwa maana ligi zinazocheza zitamenyana zenyewe kwa zenyewe Panama dhidi Sahare All Star.

Klabu ya Stand United inayoshiriki Ligi daraja la kwanza baada ya kushuka msimu uliopita itamenyana na Simba Sc.

Kunako dimba la Nangwanda Sijaona vijana wa Ndanda watakuwa nyumbani kucheza na Kitayosa Fc.

Michezo yote hii itachezwa tarehe za mwanzo ama katikati za mwezi wa pili.

Author: Bruce Amani