Droo ya Kinyang’anyiro cha AFCON 2022 kufanywa Yaounde

Droo ya king’anyiro kilichopangwa upya cha Kombe la Mataifa ya Afrika 2022 nchini Cameroon itafanywa mjini Yaounde Agosti 17. Mashindano hayo awali yalitarajiwa kuandaliwa Juni 25 katika mji mkuu wa Cameroon lakini yakaahirishwa kwa sababu ya masuala yanayohusiana na janga la virusi vya corona. Tamasha hilo la kandanda la Afrika lenye nchi 24 limeahirishwa mara mbili kwa sababu ya COVID-19 na sasa linatarajiwa kung’oa nanga Januari 9 na kukamilika Februari 6.

Algeria itatetea kombe waliloshinda Cairo miaka miwili iliyopita kwa kuwafunga Senegal 1-0 katika fainali. Cameroon wanaandaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1972, wakati nchi nane pekee zilishiriki na Congo Brazaville wakaibuka kidedea.

Nchi nyingine zilizofuzu ni Burkina Faso, Cape Verde, Cote d’Ivoire, Comoros, Misri, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Guinea ya Ikweta, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Tunisia, Sudan na Zimbabwe.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares