Droo ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

Mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya Bayern Munich watachuana na Paris St-Germain katika mchezo wa robo fainali ya Champions League msimu huu wakati Borussia Dortmund ikiwa na kibarua dhidi ya Manchester City ya Uingereza.

Chelsea inayotiwa makali na Thomas Tuchel, itachuana na klabu ya Ureno ya Porto alafu Real Madrid ya Uhispania itazipiga na Liverpool ya Uingereza.

Mechi kati ya Bayern Munich na Paris St-Germain ni marudio ya fainali ya Champions League msimu uliopita wakati Bayern ilipoifunga PSG bao 1-0, bao lililofungwa na mchezaji wa zamani wa PSG Kingsley Coman.

Fainali ya mwaka huu itachezwa mnamo Mei, 29 mwaka 2021 katika uwanja wa Atatürk Olympic mjini Istanbul, Uturuki.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares