Droo ya robo fainali ya Ligi ya Europa

605

Kitendawili cha robo fainali ya Ligi ya Europa kimeteguliwa rasmi. Baada ya hatua ya 16 bora kukamilika na kila timu kuwa gizani katika kutambua mpinzani wake katika hatua ya nane bora.

Droo hiyo imekamilika ambapo Manchester United imepangwa kupepetana vikali na Granada inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania na mechi nyingine arsenal watacheza na Slavia Prague.

Ajax watacheza dhidi ya Roma na Dinamo Zagreb itachuana na Villarreal.

Katika hatua ya robo fainali, mshindi wa mechi ya Granada na Manchester United atacheza na mshindi baina ya Ajax au Roma na mshindi wa mechi ya Dinamo Zagreb dhidi ya Villarreal atacheza na mshindi wa mechi ya Arsenal au Slavia Prague.

Mechi mbili za robo fainali zitachezwa kuanzia tarehe 8 kwa mkondo wa kwanza na mkondo wa pili itakuwa Aprili 15.

Wakati nusu fainali itakuwa tarehe 29 Aprili na 6 Mei.

Author: Asifiwe Mbembela