Dybala, Authur pasua kichwa Juventus

Kocha wa kikosi cha Juventus Andrea Pirlo hajawajumuisha wachezaji watatu wa timu yake itakayochuana vikali na Torino Kesho Jumamosi mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia kufuatia nyota hao kukiuka misingi ya kujikinga na virusi vya Corona.

Wachezaji ambao wameachwa na kocha huyo ni pamoja na Weston McKennie, Paulo Dybala na Arthur na wote wametozwa faini na klabu hiyo baada ya wote watatu kuwepo katika sherehe iliyofanyika Jumatano mwenyeji akiwa ni Mckennie.

“Wachezaji watatu waliohusika na sherehe hiyo hatujawaita kwenye mechi ya kesho, wataendelea kuwa nasi baada ya mechi” alisema kocha Pirlo Leo Ijumaa.

Pirlo yuko kwenye msimu wake wa kwanza na Juventus ingawa magazeti nchini Italia yanasema anaweza kufukuzwa kutokana na matokeo mabaya klabuni hapo baada ya mechi mbili zijazo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares