Emerging Stars ya Kenya tayari kuvaana na Sudan

Timu ya kandanda ya Kenya ya wachezaji wasozidi umri wa miaka 23 itakosa huduma za nahodha wake Joseph Okumu.

Kwa mujibu wa kocha wa vijana hao Francis Kamanzi, ni kuwa kukosekana kwake hata hivyo hakutoathiri mipango yake kwa kuwa anao wachezaji wengine wa kujaza nafasi ya beki huyo ambaye hucheza soka lake Marekani na klabu ya Real Monarchs.

Kenya inatarajiwa kuvaana na Sudan hapo kesho Jumatano jioni katika mechi ya awamu ya kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika sawa na michuano ya Olimpiki.

Mechi ya marudio itachezwa mjini Nairobi tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares