‘England hawapaswi kuwaogopa Wajerumani’ – Matthaus

Timu ya taifa ya England itacheza na taifa la Ujerumani katika kuwania kufuzu robo fainali michuano ya Euro 2020 siku ya Jumanne lakini Ujerumani wamekuwa wakipewa kipaumbele cha kushinda na lijendi wa Ujerumani anasema “hawapaswi kuogopa”.
Lothar Matthaus ameyasema hayo kuelekea mtanange wa kukata shoka wa 16 bora Euro 2020 ambapo amesema England ni timu kubwa kama ilivyo Ujerumani.
Matthaus ambaye alikuwa nahodha wa iliyokuwa Ujerumani Magharibi mwaka 1990 alipoifunga England kwa penati nusu fainali ametoa tahadhari kwa England kuwa wanapaswa kuhakikisha wanashinda kwenye dakika za kawaida kwani wakifika kwenye mikwaju ya penati Ujerumani wana historia nzuri.
“England wana nafasi nzuri ya kushinda, lakini sio kwenye penati”, alisema Matthaus.
“Siku zote Ujerumani wanahistoria nzuri kwenye penati, lazima washinde kabla ya hatua hiyo”.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares