England yavutwa nyuma na Hungary

England imebanwa mbavu na Hungary katika sare ya goli 1-1 kwenye mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022, mchezo ambao umeshuhudiwa ukigubikwa na ghasia na vurugu za mashabiki.

Kocha wa kikosi hicho Gareth Southgate akizungumzia sare hiyo amesema ‘imenivunja nguvu’.

England bado wako kwenye nafasi nzuri ya kufuzu ingawa wanatakiwa kuwa bora zaidi kufanya vizuri kutokana na kazi kubwa ya kutwaa ubingwa wa dunia hasa eneo la kumalizia.

Kwenye mechi hiyo, bao la Hungary likiwekwa kimiani na Roland Sallai baada ya beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw kumfanyia madhambi Loic Nego. Bao lililosawazishwa na Jones Stone muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends