“EPL is back” Manchester City dhidi ya Arsenal Juni 17

Hatimaye ligi pendwa nchini ulimwenguni, ligi kuu ya England imekusudia kuanza kuchezwa tena Juni 17 kwa michezo kiporo, Manchester City watakuwa nyumbani kuikalibisha Arsenal wakati Aston Villa wataivaa Sheffield United.

Licha ya kuanza kuchezwa Juni 17 lakini raundi zote zitaanza kuchezwa rasmi Juni 19-21 ambapo zaidi ya michezo 92 itachezwa ndani ya miezi miwili, zaidi ya wikiendi sita.

Usalama kwa kuchukua tahadhari za kujikinga na Covid-19 kwa wachezaji na viongozi bado umesisitizwa uendelee kuchukuliwa.

TULIPOISHIA

Utakumbuka wakati ligi ikisitishwa mwezi Marchi, mabingwa wa Ulaya Liverpool walikuwa wanaongoza mbio za ubingwa kwa tofauti ya alama 25 dhidi ya timu iliyonafasi ya pili yaani Manchester City wakati ambapo timu tatu ziko mkiani Bournemouth, Aston Villa na Norwich City.

Liverpool ambayo inafukuzia ubingwa wa kwanza baada ya miaka 30, na wanaweza kutawazwa kuwa mabingwa katika mchezo wao wa kwanza endapo Manchester City itapoteza dhidi ya Arsenal katika mchezo kiporo.

“Ligi yetu inafahamika ilivyo na utamaduni wa mashabiki wengi kupenda kuangalia mpira, tuna hakikisha kila shabiki anaangalia mpira bila kukosa akiwa nyumbani” alisema Mkurugenzi wa EPL Richard Masters.

Leo Ijumaa Shirikisho la Soka England imepanga kutangaza rasmi tarehe ya kuchezwa kwa mechi za robo fainali ya FA, nusu fainali na fainali yenyewe.

UEFA NA MPANGO KAZI

Mechi za ligi ya mabingwa na Europa hatua ya 16 imekusudia kuanza kuchezwa Agosti 6 na 8 wakati taifa la England linawakilishwa na Manchester City, Manchester United na Wolverhampton. Ligi inarudi baada ya siku takribani 100, mchezo wa mwisho ulikuwa wa Leicester City wakishinda goli 4-0 Aston Villa Marchi 9.

Viwanja huru huenda visitumike tena ili kuruhusu mechi nyingi kuchezwa kwa muda mwafaka, hata hivyo inaweza ikawa kwa sababu ya juhudi za vilabu vya West Ham, Brighton na Aston Villa kupinga utaratibu huo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends