Eriksen afika uwanjani kwa mara ya kwanza

Kiungo mshambuliaji wa Inter Milan Christian Eriksen amesema kuwa kwa sasa anaendelea na kujisikia vizuri baada ya tukio la kupoteza fahamu uwanjani kwenye mechi yao ya kwanza ya michuano ya Euro 2020 dhidi ya Finland.

Eriksen ameyasema hayo baada ya kuwasili viwanja vya mazoezi vya klabu ya Inter Milan na kuwaeleza wachezaji wenza na viongozi kuwa anajisikia vyema ingawa anaendelea na matibabu kabla ya kurejea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa 29, alifika uwanjani hapo Jana Jumatano Agosti 4 na baada ya mazungumzo ya pamoja walipiga picha ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu nzuri kwa mchezaji huyo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends