Eriksen atua Inter Milan akitokea Spurs

Inter Milan imekamilisha dili la kumsajili kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Christian Eriksen kwa dau la pauni milioni 16.9.

Eriksen, 27, ameingia kandarasi ya mpaka mwaka 2024 Juni 30.

Shinikizo ambalo kiungo huyo raia wa Denmark aliliweka kwa viongozi wa Spurs la kuhitaji kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kupata changamoto mpya ndilo lililopelekea kuondoka kwa dau la chini kabisa.

Awali Eriksen alikusudia kwenda Hispania katika klabu ya Real Madrid baada ya kuhusishwa nae lakini tangu wasitishe uhitaji wake aliamua kuichezea Tottenham msimu huu ambapo amecheza jumla ya mechi 28 katika mashindano yote.

Inter wapo katika harakati za kupindua utawala wa Juventus ndani ya Seria A wanajitahidi kujiimarisha ili kuendeleza timu bora ya kushindana na Juve iliyonafasi ya kwanza wakati Inter ikiwa ya pili kwenye msimamo wa Seria A.

“Siku zote huwa ni furaha kwa kila mchezaji kucheza katika klabu kongwe yenye historia bora duniani, hata mimi najiona mwenye bahati kuwa sehemu ya timu hii”.

Takwimu zangu zinaonyesha nimefanya vizuri nikiwa England. Sasa ni wakati wangu kupata changamoto mpya hapa, nina furaha kupata nafasi ya kucheza na miongoni mwa wachezaji bora pia” alisema Eriksen ambaye ni miongoni mwa wachezaji wachache wenye jicho la goli la pasi za mwisho.

Wakati Eriksen akiondoka Tottenham imekamilisha usajili wa kiungo aliyekuwa anakipiga kwa mkopo klabuni hapo Giovani Lo Celso aliyetokea Real Betis.

Unakuwa mchezaji wa tano kutua Inter kutoka EPL msimu huu baada ya Ashley Young, Romelu Lukaku, na Alexis Sanchez (mkopo), na Victor Moses (mkopo)

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends