Esperance kukwaruzana na Wydad fainali ya Ligi ya Mabingwa

57

Esperance de Tunis ya Tunisia, itamenyana na Wydad Casablanca ya Morocco katika fainali ya kuwani taji la klabu bingwa barani Afrika.

Hii imefahmaika baada ya mzunguko wa michuano ya nusu fainali kuchezwa Jumamosi jioni

Baada ya kufungwa ugenini bao 1-0 wiki iliyopita, TP Mazembe wakicheza nyumbani, wameshindwa kufungana na wageni wao Esperance de Tunis, na mambo yamekuwa hivyo kule Afrika Kusini, baada ya wenyeji Mamelodi Sundowns waliokuwa wamefungwa mabao 2-1 na Wydad Casablanca, kushindwa kupata ushindi.

Mzunguko wa kwanza wa fainali, utachezwa tarehe 24 nchini Tunsiia kabla ya ile ya mwisho kuchezwa tarehe 31 mwezi huu.

Author: Bruce Amani