Habari za hivi karibuni

  • Bosi wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino amedai kwamba kilabu haikumpa muda wa kuleta mabadiliko kikosini. MuArgentina huo pia alisema kwamba kilabu ilipoteza imani katika maono yake kufuatia “makosa” aliyofanya. Pochettino alifurushwa Novemba mwaka jana … Read More

  • Madai ya Gianni Infantino kuwa siku za ufisadi katik FIFA zimezikwa katika kaburi la sahau yamepata pigo kufuatia uchunguzi wa jinai unaofanywa dhidi ya rais huyo wa shirikisho la kandanda ulimwenguni. Patashika Viwanjani leo inakufahamisha … Read More

  • Timu ya mawakili wa Gianni Infantino imelaani uchuguzi wa uhalifu unaofunguliwa na wapelelezi wa Uswisi. Uchunguzi huo unahusu mkutano kati ya rais huyo wa FIFA na Mwanasheria Mkuu wa Uswisi Michael Lauber. Katika kikao cha … Read More

  • Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia miaka miwili aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael kujihusisha na masuala ya soka nchini Tanzania. Mbali na kufungiwa miaka miwili pia TFF imemtaka kocha … Read More

  • Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na mechi za Ligi ya Europa League zinarejea tena wiki hiii huku timu zikiwania tiketi ya kufuzu kwa robo fainali ya michuano hiyo. Ijumaa itakuwa ni zamu ya mabingwa wa Serie A Juventus kuchuana na Olympic Lyon ya Ufaransa huku Manchester City ya England ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya mabingwa wa Uhispania Real Madrid halafu siku ya Jumamosi Barcelona itapambana na Napoli nayo Bayern Munich itaialika Chelsea katika uwanja wa Allianz Arena. Hata hivyo, kuna hali ya ati ati iwapo Barcelona itaruhusiwa kuutimia uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp kutokana na hofu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona jimboni Catalonia. Washindi wa mechi hizo watajiunga na Paris Saint Germain, Atletico Madrid, RB Leipzig na Atalanta ambazo tayari zimefuzu katika hatua ya robo fainali. Europa League Na katika mechi za Europa League, Jumatano hii Manchester United itaingia uwanjani kuvaana na LASK ya Austria, ilhali Inter Milan itakuwa katika uwanja wa Veltins Arena kukabana koo na Getafe ya Uhispania. Mechi nyengine za Europa League zinaikutanisha Shakhar Donestk na Wolfsburg huku Copenhagen ikichuana na Istanbul Basak-sehir.

  • Nguli wa kandanda aliyewapa burudani mashabiki wa Chelsea dimbani Stamford Bridge Didier Drogba amejitosa rasi katika kinyang’anyiro cha Urais wa chama cha soka cha Ivory Coast. Drogba mwenye umri wa miaka 42, ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Afrika ni miongoni mwa wagombea wanne wanaotafuta ridhaa ya kukiongoza chama cha soka katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Hata hivyo, hana uhakika iwapo atashiriki katika uchaguzi huo uliopangwa Septemba 5. Pamoja … Read More

  • Meneja wa Chelsea Frank Lampard anaamini kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu nchini England Septemba 12 ni mapema mno katika kufanya maaandalizi ya msimu. Frank Lampard anatoa malalamiko leo wakati ambao ratiba ya msimu wa … Read More

  • Mshindi wa Kombe la FA Arsenal imekusudia kumvuta beki wa kati wa Sevilla Diego Carlos, 27, ambapo kocha Mikel Arteta amepanga kuboresha kikosi chake eneo la ulinzi. Ripoti nyingine zinaeleza kuwa Arteta anafanya mazungumzo ya chini kwa … Read More