European Super League yaiponza Man United, City, Chelsea Liverpool adhabu kali yawatembelea

Klabu sita kutoka nchini England zilizokubali kujiunga na mashindano mapya ya European Super League (ESL) zimepigwa faini pamoja na kupewa masharti kibao kutokana na nia yao hiyo.

Klabu ambazo zilikubali kuingia kwenye michuano hiyo mipya ingawa baadaye zilijitoa ni klabu kubwa Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester United, Manchester City na Tottenham Hotspur.

Ambapo Chama cha Soka England kwa kushirikiana na Uefa kimetoa adhabu ya kiasi cha pauni milioni 22 kama faini ya usumbufu kwa wadau, madhamini wa Ligi ya ndani huku wakipewa masharti ya kutorudiana tena, na endapo itajitokeza basi watalipa pauni milioni 25 kila klabu pamoja na kupokwa pointi 30.

Uefa kwa sasa imesitisha kwa muda, kujadili masuala ya kinidhamu kwa klabu za Real Madrid, Barcelona na Juventus ambazo bado hazijatangaza kujitoa katika umoja huo wa ESL.

Ni klabu tatu pekee kutoka kwenye zile 12 ambazo hazijatangaza kujitoa lakini pia hazikubali kulipa faini yoyote kutokana na usumbufu huo tangia mwezi Mei mwaka huu.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares