Everton wawazuia Liverpool kukamata usukani wa ligi

Huenda baada ya refarii kupuliza kipyenga cha mwisho, upande wa samawati wa jiji la Manchester ulishangilia kwelikweli. Everton ilihakikisha kuwa Manchester City inasalia kileleni mwa Ligi ya Premier baada ya kuonyesha mchezo wa kijasiri na kuwateka Liverpool kwa sare tasa katika dimba la Goodison Park.

Liverpool ilihitaji ushindi ili kuwapiku City baada ya ushindi wao dhidi ya Bournemouth lakini vijana hao wa kocha Jurgen Klopp walikosa mbinu na ujanja wa kupenya katika ngome imara ya Everton katika mtanange mkali wa Merseyside derby.

Kipa wa Everton Jordan Pickford, ambaye katika mtanange wa Anfield Desemba mwaka jana, alimzawadi Divock Origi bao katika dakika ya 96, ndiye aliyekuwa shujaa alipookoa komboa la Mo Salah katika kipindi cha kwanza.

Manchester City sasa wanaongoza ligi na pointi 71, moja mbele ya Liverpool huku zikisalia mechi tisa msimu kukamilika. Everton wanabaki nafasi ya 10.

Fulham 1 – 2

Jorginho amefunga bao lake la kwanza kwenye ligi

Kocha wa Chelsea anaonekana kuwa amerejea tena kutoka ukingoni, Jorginho amepiga hatua moja mbele kwa kufunga bao la ushindi na Kepa Arrizabalaga aliyaweka kando masaibu ya Wembley.

Zimekuwa siku kumi zenye mambo chungu nzima kwa Chelsea. Sari alionekana kuwa karibu na shoka la kufutwa kazi, lakini ameshinda derby ya pili mfululizo na sasa timu yake imesogea karibu na nafasi nne za kwanza kwa kupungukiwa na pointi mbili tu huku wakiwa na mechi moja ya ziada na pointi tano tu nyuma ya nambari tatu Tottenham Hotspur.

Gonzalo Higuain aliifungia Chelsea bao la kwanza kabla ya Calum Chambers kuisawazishia Fulham ambayo inaongozwa na kocha wa muda Scott Parker, baada ya Claudio Ranieri kutimuliwa. Jorginho aliifunga la pili na kuhakisha kuwa Chelsea wanapata pointi zote tatu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends