Everton, West Ham zagongana kusaka huduma ya Edin Dzeko

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko, 32, amepanga kuondoka ndani ya klabu ya Roma ya Italia baada ya kushindwa kuelewana na bosi wake Paulo Fonseca. Matamanio ya kuondoka kwa mchezaji huyo ndani ya Roma kumeziamusha timu za Everton na West Ham United ambazo zinatajwa kuwania saini ya strika huyo matata.

Wagonga Nyundo wa London klabu ya West Ham imeiomba klabu ya Manchester United kumwachia kiungo mshambuliaji wa timu hiyo raia wa England Jesse Lingard, 28, kufuatia kukosa nafasi ya kucheza Manchester United.

Manchester United wanaendelea na mazungumzo ya kumsajili fowadi wa Kibrazil na Palmeiras Gabriel Veron, 18, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Manchester City, Barcelona na Juventus.

Bosi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anatamani kuungana tena na kiungo mshambuliaji wa Tottenham Dele Alli, 24, licha ya ofa tatu kupigwa chini na klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya Jose Mourinho.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares