Everton yafundishwa kandanda na Leeds United ya Bielsa

14

Kikosi cha kocha Marcelo Bielsa kimefanikiwa kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli 1-0 mbele ya Everton ambayo inanolewa na kocha Carlo Ancelotti, bao pekee la Raphinha likileta utofauti wa matokeo baina ya timu hizo mbili.

Bielsa anakiongoza kikosi chake kushinda mechi ya nne tangu apande na timu Ligi Kuu nchini England kutokea daraja la pili.

Winga huyo raia wa Brazil alijiunga na Leeds mwezi Octoba akitokea Rennes ya Ufaransa mpira wake ulimpita mlinda mlango wa Everton Jordan Pickford. Leeds wanakwea mpaka nafasi ya 11 kwenye msimamo wa EPL wakati Everton wanasalia nafasi ya sita.

Author: Asifiwe Mbembela