Everton yatinga robo fainali Kombe la FA England baada ya kuifunga Spurs katika mtanange wa mabao tisa dimbani Goodison park

Everton wametinga hatua ya robo fainali ya Kombe la FA nchini England kwa kuifunga Tottenham Hotspur goli kupitia mikwaju ya penalti 5-4 katika mchezo uliopigwa dimba la Goodison Park Jana Jumatano.

Ukiwa mchezo wa aina yake, Tottenham inayonolewa na kocha Jose Mourinho ilitangulia kupata bao kupitia kwa Davinson Sanchez, kabla ya mshambuliaji wa kati wa Everton Dominic Calvert-Lewin kusawazisha, Richarlison akaongeza la pili na la tatu kwa Everton likifungwa na Gylfi Sigurdsson kwa penati.

Eric Lamela alirudisha matumaini kwa Spurs kwa kufunga bao na kufanya 3-2, Sanchez alirudi tena nyavuni, Kane akaongeza lingine tena, lakini Richarlison aliingia kambani.

Everton walirudi tena kwa kufunga goli kunako dakika za ziada na Bernard akimalizia pasi ya Sigurdsson.

Mpaka mpira unamalizika Everton wenyeji bao 5-4 kwa Tottenham na hivyo kutupwa nje ya mashindano hayo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares