Fabinho ajifunga Liverpool mpaka 2026
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Fabinho ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kutumika ndani ya klabu hiyo, sasa mkataba wake kufikia tamati 2026.
Mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 amecheza mechi 122 ndani ya Liverpool akitumika kama mlinzi wa kati msimu uliopita baada ya changamoto ya majeruhi.
Anakuwa mchezaji wa pili kuongeza mkataba mpya baada ya beki wa kulia wa England Trent Alexander-Arnold, ambaye aliongeza mkataba mpya wiki iliyopita.
“Ni kitu ambacho nakihitaji, nahitaji kuendelea kusalia hapa maana nina furaha”, alisema mchezaji huyo wa zamani wa Monaco.