Falcao atua Rayo Vallecano akitokea Galatasaray

Mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao amekubali kujiunga na klabu ya Rayo Vallecano baada ya kuondoka Galatasaray Jumatano ya wiki hii.
Falcao mwenye umri wa miaka 35, anarejea kwenye La Liga baada ya miaka nane itakumbukwa amewai kucheza ndani ya Atletico Madrid.
Akiwa Atletico, Falcao alishinda taji la Copa del Rey, Europa League na Uefa Super Cup.
Alijiunga na Monaco mwaka 2013 ambapo amewai kutumika pia Manchester United na Chelsea katikati ya mwaka 2014 na 2016 kabla ya kukimbilia Galatasaray kwa mkataba wa kudumu.
Alifunga goli 19 katika mechi 34.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares