Feeney awataka Shujaa kujiimarisha zaidi katika ulinzi

Kocha mkuu wa timu ya raga ya Kenya Paul Feeney anataka Shujaa kumakinika upande wa Ulinzi, na kupiga mikiki kabla ya michuano ya raga ya Dubai Sevens mwezi ujao. Mzaliwa huyo wa New Zealand, ambaye alichukua usukani miezi mwili iliyopita, aliisaidia Kenya kufuzu katika michezo ya Olimpiki mjini Tokyo 2020 wikendi iliyopita mjini Joburg. Kenya itarejea mazoezini wiki ijayo kabla ya kupambana na Uingereza, Uhispania na Dubai mwezi Ujao.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends