Feisal awaka moto, Yanga yaichapa KMC Ligi Kuu

Kiungo mshambuliaji wa Kitanzania Feisal Salum “Fei Toto” amehusika kwenye goli zote mbili kwenye ushindi wa goli 2-0 walioupata Yanga mbele ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Tanzania, mtanange uliopigwa dimba la Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Feisal Salum Abdallah alifunga goli la pili lakini awali alikuwa amemsaidia bao mshambuliaji wa timu hiyo Fiston Mayele magoli yote yakifungwa kipindi cha kwanza ndani ya dakika 11 za kwanza.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha alama tisa baada ya mechi tatu na sasa ndiyo kinara wa Ligi Kuu ya NBC.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends