Fernandes, Ronaldo watu pia kwa Ureno ikiichapa Israel bao 4-0

Maandalizi kwa timu ya taifa ya Ureno yamekamilika kwa furaha kuelekea kwenye mashindano ya Euro 2020 kufuatia kuibuka na ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya taifa la Israel mchezo uliopigwa Jana Jumatano.

Magoli ya Ureno inayoongozwa na nahodha Cristiano Ronaldo yalifungwa na kiungo mshambuliaji wa Manchester United Bruno Fernandes aliyefunga goli mbili, Ronaldo goli moja pamoja na beki wa Man City Joao Cancelo.

Ureno ambao wanaingia kwenye michuano hiyo kama Mabingwa watetezi wataanza kampeni ya kutetea taji hilo siku ya Jumanne Juni 15 dhidi ya Hungary.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares