FIFA kuchunguza ripoti ya upangaji matokeo ya mechi za Kenya

20

Shirikisho la soka duniani FIFA, limethibitisha kuwa linachunguza ripoti ya kuwepo kwa matukio ya kupanga matokeo ya mechi za timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, katika miaka iliyopita.

Hatua hii ya FIFA imekuja baada ya ripoti ya uchunguzi ya Gazeti la kila siku nchini humo la Daily Nation, kuripoti kuwa beki za zamani George Owino alihusika na kosa hilo kati ya mwaka 2009 mwezi Juni hadi Machi mwaka 2011.

Indaiwa kuwa mchezaji huyo na wengine watatu ambao hawajatambuliwa walilipwa Mamilioni ya pesa za Kenya na raia wa Singapore, Raj Perumal ili kusababisha Harambee Stars kushindwa wakati wa michuano ya Kimataifa.

Kanuni za FIFA zinaeleza kuwa, mchezaji au mtu yeyote anayebainika kuwa alihusika na kosa la upangaji wa matokeo, ataadhibiwa kwa faini ya Dola 100,000 na kufungiwa kutoshiriki katika masuala ya soka kwa angalau miaka mitano.

Author: Bruce Amani