FIFA yajitolea kuwasaidia wachezaji wasiolipwa mishahara

Shirika la Kandanda Ulimwenguni – FIFA linazindua mfuko wa kuwasaidia wachezaji ambao hawajalipwa na vilabu vyao. Mfuko huo wa dola milioni 16 utaanza kutumika kuanzia Julai mosi na kuhudumu hadi 2022 kwa makubaliano na chama cha wachezaji wa kulipwa duniani FIFPRO. Dola milioni 5 kutoka kwenye mfuko huo zimetengwa kwa ajili ya ulinzi wa mishahara ya wachezaji kati ya Julai 2015 na Juni 2020. Taarifa ya FIFA imesema kumekuwa na kesi za wachezaji ambao hawajalipwa mishahara kote duniani. Rais wa FIFPRO Philippe Piat amesema zaidi ya vilabu 50 katika nchi 20 vimefungwa katika miaka mitano iliyopita, na kuwaweka mamia ya wachezaji kandanda katika hali ya sintofahamu na taabu.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments