FIFA yapendekeza kurefushwa mikataba ya wachezaji

53

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limependekeza kurefushwa kwa mikataba ya wachezaji ambayo ilipaswa kukamilika mwezi Juni na kusema kuwa litaruhusu madirisha ya usajili wa wachezaji kuhamishwa ili kuruhusu kurefushwa kwa msimu wa sasa wa kandanda la Ulaya kutokana na janga la COVID-19. FIFA pia imesema kuwa itavihimiza vilabu na wachezaji “kushauriana ili kufikia makubaliano na suluhisho wakati wa kipindi ambacho mashindano yamesitishwa na kuwa mchezo wa kandanda unapaswa kukabiliana na hasara isiyo ya kawaida ya mapato. Virusi vya corona vimesitisha shughuli za kandanda kote duniani, huku ligi za kitaifa zikisitishwa kwa muda na mashindano makuu kama vile Euro 2020 na Copa Amerika, yakiahirishwa hadi mwaka ujao. Shirikisho la Kandanda Ulaya – UEFA limesema linataka msimu wa 2019-2020 ukamilishwe uwanjani, hata kama ina maana kuurefusha hadi Agosti.

Author: Bruce Amani